Loading...

Mambo manne yaliyoafikiwa kwenye kikao cha dharura kuhusu kusudio la Manji kujitoa Yanga

 
August 16 2016 ikiwa ni siku moja imepita toka kuenea kwa habari katika mitandao ya kijamii kuwa mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa madai ya kuandamwa na maneno na kujihisi mpweke kwani hakuna mwanachama yoyote wa Yanga aliyeonesha kuwa upande wake.
Baada ya taarifa hizo kuenea viongozi wa kanda wa Yanga walikaa na kuamua kufanya mkutano wa dharura leo August 16 makao makuu ya klabu yao,  moja kati ya viongozi wa matawi ya Yanga mkoa wa Dar es Salaamanayeiwakilisha kanda ya Temeke Robert Liungu ametaja maazimio waliyofikia kutoka katika mkutano wa dharura.
1- Wanachama wa Yanga wanatambua kuwa Manji bado ni mwenyekiti wao kwa mujibu wa katiba yao.
2- Wanachama wamemuomba mdhamini Mzee Katunda amtoe mzee Akilimali anayedaiwa kumpinga Manji atolewe katika nafasi ya katibu wa wazee wa Yanga.
3- Wanachama wanaiomba kamati ya utendaji ya Yanga imuite mzee Akilimali imuhoji na kumsimamisha uanachama kwa madai kuwa yeye ni Simba. 
4- Wanachama wa matawi yote wanaendelea kumtambua Yusuph Manji kama mwenyekiti wao

Fununu Za Yanga Zilizosambaa Mitandaoni MANJI ndiyo Basi Tena

Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa yanga pamoja na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake .
Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Bw Yusuf Manji atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu Bw mohamed Dewji MO.
Uamuzi wa manji kujiondoa yanga unatajwa kuchangiwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya yanga.
Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake .
Hata hivyo viongozi wa Secretary ya yanga siku nzima ya leo wameonekana kuchanganyikiwa uku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka quality plaza zilizopo ofisi za Bw manji hatua inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.

Breaking News: MANENO YA WATU SUMU...CLUB YA YANGA YAPATA PIGO ZITO SIKU YA LEO

Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga SC, wametupwa nje kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya TP Mazembe kuchapwa mabao 3-2 na Medeama ya Ghana katika mchezo wa kundi A uliofanyika kunako dimba la Essipong Sports huko Takoradi, Ghana.

Medeama walipata mabao yao kupitia kwa Enock Atta Agyei, Moses Amponsah Sarpong na Kwesi Donsu huku Mazembe wakipata mabao yao yote mawili kupitia kwa Jonathan Bolingi.

Kufuatia matokeo hayo, Medeama ambao mchezo wa mwisho watacheza na MO Bejaia watahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali, wakati huo Yanga watakuwa ugenini wakikipiga na TP Mazembe mjini Lubumbashi, mchezo ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba tu kwa upande wa Yanga.

Mpaka sasa, TP Mazembe bado wako kileleni na pointi zao 10 baada ya michezo mitano, wakishinda mara tatu, sare mara moja na kufungwa mara moja, wakifuatiwa kwa karibu na Medeama wenye alama nane, Bejaia wakishika nafasi ya tatu na pointi zao tano na Yanga wakiburuza mkia na pointi zao nne.

Hata kama Yanga itashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mazembe, haitasaidia chochote katika kufuzu hatua ya nusu fainali kwasababu watafikisha pointi saba wakiwa wamemaliza mechi zote wakati Medeama tayari wamefikisha pointi nane ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga.

Mchuano mkali umebaki kati ya Medeama na Bejaia mabapo kila timu inasaka nafasi ya kuungana na Mazembe kuelekea nusu fainali huku Mazembe pia ikihitaji kushinda ili kuongoza Kundi lao la A.
Older Posts
© Copyright CHUNGU CHETU | Designed By CHUNGU CHETU
Back To Top