Washtakiwa hao ambao ni viongozi na wafuasi wa Uamsho walikuwa wakisafirishwa katika basi la Magereza lililokuwa likisindikizwa magari aina ya Land RoverDefender zilizokuwa zimejaa askari wenye silaha na baadhi yao wamejifunga vitambaa vyeusi usoni.
Risasi hizo ziliwatawanya ndugu wa washtakiwa hao wanaofika na kukaa nje kila kesi hiyo inapotajwa walipotaka kusogelea msafara huo.
Washtakiwa hao ni Sheikh Farid Hadi Ahmed, mkazi wa Mbuyuni; Noorid Swalehe wa Fundi ujenzi , mkazi wa Koani na Jamal Nooridin Swalehe.
Wengine ni Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.
Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu.
Inadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 walipanga njama za kusaidia na kuwezesha kufanyika kwa vitendo vya kigaidi.
Post a Comment