Hivi karibuni, ilibainika kuwapo kwa wanafunzi hewa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini kote, hali iliyosababisha serikali kuamuru uhakiki wa wanafunzi kufanyika upya.
Kutokana na shaka hiyo ya matumizi ya fedha katika akaunti namba 0150221323700 iliyoko katika benki ya CRDB, PAC imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na mwenendo wa matumizi yake.
Agizo hilo lilitolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi Hilary, alipokuwa akitoa maagizo ya kamati hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi, baada ya kupitia ripoti ya CAG.
Hilary alisema ripoti hiyo inaonyesha matumizi mabaya ya fedha ambazo zilitumika bila kufuata kanuni na taratibu, yakiwamo matumizi Sh. bilioni 1.2.
Alisema matumizi hayo ni pamoja na Wizara kutumia zaidi ya Bilioni 1.2 kwa ajili ya maandalizi ya hafla ya kuchangisha dola milioni tatu (zaidi ya Sh. bilioni sita), ambayo ingefanyika Marekani kwa ajili ya kubuni na kutengeneza mbinu za ufundishaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika shule za sekondari nchini.
Aliongeza kuwa pamoja na matumizi ya kiasi hicho cha fedha, hakuna mafanikio yoyote kwa kuwa hafla hiyo haikufanyika, hivyo mabilioni hayo kupotea bure bila kuwa na tija kwa serikali.
“Kamati inamwomba CAG afanye uhakiki katika mwenendo mzima wa akaunti hii na kutoa taarifa ya matumizi ya fedha za wizara ambazo zimetumika.” alisema.
Alisema Katibu Mkuu anatakiwa kuwasilisha mchanganuo wa fedha pamoja na wahusika ili kubaini watu waliohusika katika matumizi hayo na kwamba taarifa hiyo iwasilishwe kwa Katibu wa Bunge kabla ya Septemba Mosi, mwaka huu.
Aidha, alisema kamati imemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kupitia kwa kina ujenzi wa jengo la wizara hiyo lililotakiwa kujengwa mkoani Dodoma, uliosababisha kulipwa kwa Sh. milioni 780.6 bila kufuata sharia ya ununuzi wa umma. Fedha hizo zililipwa kwa kampuni ya Prison Corporation kabla ya kutiwa saini mkataba.
Sambamba na hilo, katibu mkuu ametakiwa kuwachukulia hatua watumishi wote waliohusika na taarifa ya utekelezaji iwasilishwe kwa kamati hiyo kabla ya Septemba Mosi.
“Pamoja na kuonekana wizara imefanya malipo ya kiasi hicho cha fedha, hakuna kitu chochote kilichofanyika hadi sasa kwani hata kiwanja ambacho kilitakiwa kujengwa jengo hilo kwenye ripoti hakionekani kilipo,” alisema.
Post a Comment