August 16 2016 ikiwa ni siku moja imepita toka kuenea kwa habari katika mitandao ya kijamii kuwa mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa madai ya kuandamwa na maneno na kujihisi mpweke kwani hakuna mwanachama yoyote wa Yanga aliyeonesha kuwa upande wake.
Baada ya taarifa hizo kuenea viongozi wa kanda wa Yanga walikaa na kuamua kufanya mkutano wa dharura leo August 16 makao makuu ya klabu yao, moja kati ya viongozi wa matawi ya Yanga mkoa wa Dar es Salaamanayeiwakilisha kanda ya Temeke Robert Liungu ametaja maazimio waliyofikia kutoka katika mkutano wa dharura.
1- Wanachama wa Yanga wanatambua kuwa Manji bado ni mwenyekiti wao kwa mujibu wa katiba yao.
2- Wanachama wamemuomba mdhamini Mzee Katunda amtoe mzee Akilimali anayedaiwa kumpinga Manji atolewe katika nafasi ya katibu wa wazee wa Yanga.
3- Wanachama wanaiomba kamati ya utendaji ya Yanga imuite mzee Akilimali imuhoji na kumsimamisha uanachama kwa madai kuwa yeye ni Simba.
4- Wanachama wa matawi yote wanaendelea kumtambua Yusuph Manji kama mwenyekiti wao
Post a Comment