Dar es Salaam. Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitoza faini ya jumla ya Sh19 milioni, vituo viwili vya televisheni, Clouds na ITV kwa makosa tofauti.
Katika faini hizo, Televisheni ya Clouds imeonywa na kutozwa Sh4 milioni kwa kuonyesha picha za wanawake walio nusu uchi na pia imeitoza Redio Clouds Sh5 milioni kwa kukiuka kanuni za utangazaji huku ikiitoza ITV Sh10 milioni kwa kurusha kipindi kilichomkariri mbunge akimkashifu naibu spika.
Akitoa uamuzi huo jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mapunda alisema Mei 22 kipindi cha Hip Hop kilichorushwa na Televisheni ya Clouds kilionyesha wimbo wa msanii MwanaFA ambao uliwaonyesha wanawake wakiwa nusu uchi. “Nyimbo zilidhalilisha utu wa mwanamke na zilirushwa muda ambao idadi kubwa ya watazamaji ni watoto jambo ambalo linaweza kusababisha waige tabia mbaya,” alisema.
Katika uamuzi huo, kamati ilisema kituo hicho pia kilirushwa wimbo wa Lil Bebbie unaoitwa ‘Break it Down’ ambao ulikuwa na wanawake waliovaa mavazi ya kuogelea wakiwa nusu uchi.
Post a Comment