Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo
cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf
Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa yanga pamoja na
kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya
Yanga na nembo yake .
Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Bw Yusuf Manji
atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi
Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu Bw mohamed Dewji MO.
Uamuzi wa manji kujiondoa yanga unatajwa kuchangiwa na
shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine
kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa
maslahi yao binafsi na sio ya yanga.
Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu
kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa
ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake .
Hata hivyo viongozi wa Secretary ya yanga siku nzima ya
leo wameonekana kuchanganyikiwa uku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo
kuingia na kutoka quality plaza zilizopo ofisi za Bw manji hatua
inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.
Post a Comment